Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine
wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo
hazifurahishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano,
utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza
wanaume wao ama zinawachukiza.
Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake
ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha
yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya
muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na
aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.
1. Mwanamke anayekuganda nguoni
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya
jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye
amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua.
Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa
mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake
haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila
wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.
2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na
mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana
na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya
kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni
kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani,
mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako.
Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na
marafiki zako, vilabuni, wanjani...nk, yaani kiufupi kila uendapo
anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli
huyu?
3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili
wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume
ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye
unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe
itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata
kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na
kukuacha kwenye giza.
4. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote
ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba
msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo
alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya
mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu
mzuri wa kuishi naye hata mara moja.
5. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu
hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi
kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake
ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke
haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.
6. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye
atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho
anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia
inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina
hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake
kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina
hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.
7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki
kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile
ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni
gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii
ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia
kichwani na wao kujifanya mabosi.
8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika
mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya
wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani
basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya
wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani,
bila hata kufikiria wenzao.
9. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila
wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza
kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze
chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda
wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu
nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila
anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona
mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye
ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye
mara moja.
10. Asi na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii
ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza
kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo
lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza
kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda
unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake
iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe
ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke
asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.
11. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na
chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya
mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.
12. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza
wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa
sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake
ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla
kuwauliza wazazi wake.
Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa
chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu
kutatua.
By Nesi Mapenzi
0 comments:
Post a Comment