Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha
XXL kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa
vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.
Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi
hicho hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy
amewahi kuzifanya ili kuomba wayamalize.
Hitmaker huyo wa Wanjera amesema katika urafiki wao wote na Diamond,
ni yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna
wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa
vinavyohusiana na kazi.
Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni
pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba
ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake Tupogo na
kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King
Malou. Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta
Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake
‘Number 1’ katika studio za MJ Records.
“Nikajiuliza kuwa pengine labda alikuwa na wazo kama hilo, sikutaka
kujiuliza mengi, unajua sometimes ukijiuliza mengi utaenda far zaidi,
nikauchuna tu,” alisema Ommy.
Anasema baadaye alisikia akimuambia Marco Chali kuwa amchomee CD
kwakuwa anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo
lakini Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimdanganya tu producer huyo wa
MJ Records na kwamba hakuna safari yoyote.
“Kesho yake naona anapost picha yupo kwenye ndege, nikajiuliza ‘huyu
si nilimuuliza jana kama anasafiri, si ni mwanangu’, nikasema anyway
labda ni safari imejitokeza ghafla you never know,” ameeleza Ommy.
Baadaye mshkaji wao Halima Kimwana alikuja kumwambia kuwa Diamond
alienda Afrika Kusini kufanya video yake kitendo kilichomwacha na
maswali mengi lakini anadai alipuuzia. Amesema baada ya muda ndipo
Diamond alipofanya uzinduzi wa video ya Number 1 na yeye mwenyewe
kualikwa.
Amesimulia tukio jingine ambalo lilimuumiza ni baada ya kumuomba
Diamond waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake
mwenyewe ili amsaidie kumtafutia connection.
“Sasa kila siku nikiuliza safari lini naona mtu anaingilia huku anatokea huku.”
Anadai swahiba wake huyo aliendelea kumchenga hadi alipokuja kugundua
amesafiri bila kumwambia na siku hiyo akawa hapokei simu zake. “Baada
ya kupita masaa mengi, jioni anakuja kunicheck yuko transit South Africa
‘mwanangu ilitokea ghafla nikasafiri.’ Kwahiyo nikajiuliza nikasema
hapa kuna style za kupunguzwa. Kibinadamu unajua lazima uchekeche.”
Ommy pia alielezea jinsi ambavyo alikuwa mtu wa kwanza afanye collabo
na Davido na alikuwa tayari kutoa $3,000 lakini baadaye Sallam, meneja
wa Diamond, alikuja kumweleza kuwa Dangote yupo tayari kutoa $5,000 ili
wafanye naye. Anasema aliachana na collabo hiyo na kutafuta nyingine na
Iyanya ambayo nayo pia alikuja kugundua baadaye rafiki yake huyo
ameshaiwahi.
Hata hivyo Ommy amedai kuwa kitendo cha yeye kumtumia Wema Sepetu
kwenye video ya Wanjera ilikuwa kama sababu tu ya Diamond kuvunja
ushkaji wake. Amesema ni kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla
ya kukutana na Chibu na kwamba hadi ‘first kiss’ yao aliishuhudia kwa
macho yake.
Ommy ambaye jina lake ni Omari Nyembo, amesema kukosana kwao hakukuwa
sababu ya yeye kumchukia pia Wema kwakuwa urafiki wao haukusika na
kwamba kipindi Ommy anaenda SA kufanya video hiyo, Wema alikuwa na
uhusiano na mwanaume mwingine na kukanusha kuwahi kutoka naye kimapenzi.
“Kwahiyo nikaona kuna suala lilikuwa kwamba mtu ametafuta sababu.
Hebu niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo
hii bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio
imekuwa tatizo?” amehoji staa huyo.
Kuhusu tuhuma za kutaka ‘kupumuliwa’ zilizotolewa na Diamond kwenye
post yake ya Instagram dhidi yake, Ommy amesema pale ‘mtu anapotaka
kukutana hakuchagulii tusi.’
“Sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi
gani, pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu
ataichukua ile kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza
kuzima comments zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma
comments utaona kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long
as mimi ninajua mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza
kutukanwa mimba!”
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment