Jose Mourinho alivyojibu swali kuhusu uwezekano wa kumsajili Lionel Messi

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho Jumatano ya November 23 2016 kuelekea mchezo wa Europa League dhidi ya Feyenoord katika uwanja wa Old Trafford, aliamua kufanya press conference na waandishi wa habari.
Mourinho aliongea na vyombo vya habari na kuongea vitu vingi ikiwemo mpango wao wa kutumia kipengele kilichopo katika mkataba wa Zlatan kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja, swali lakaja kuhusu uwezekano wa wao kuwa katika mpango wa kumsajili Lionel Messi kutoka FC Barcelona.
3ab0625f00000578-3965012-image-a-13_1479917614699
Swali hilo lilikuja baada ya vyombo vya habari vya Hispania kutangaza kuwa Man United wanataka kuwatumia Adidas ambao ni wadhamini wa Man United na Lionel Messi ili kumpata kirahisi.
“Kila mwaka huwa ni stori hizo hizo kila mwaka kuwa ataondoka na haondoki, naamini kamwe hawezi kuhama FC Barcelona, Messi ni kwa ajili ya Barelona na Barcelona ni kwa ajili ya Messi” >>> Jose Mourinho
Share on Google Plus

About tanzania gospel music

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment